Afarah suleiman, Babati – Manyara.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Babati CPA. Shaban Mpendu amesema ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Mji Babati (Mrara) kwa sasa umefikia asilmia 98 na wanatarajia kuanza kutoa huduma kwenye majengo hayo mwishoni mwa wiki hiii kwa kuwa Vifaa Tiba vyote vimekamilika.

CPA. Mpendu amesema hayo mara baada ya mradi huo kutembelewa na kamati ya Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kukagua majengo hayo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.4.

Amesema kukamilika kwa majengo hayo kwa wakati kumetokana na ufuatiliaji wa karibu pamoja na ushirikiano kati ya Ofisi ya Halmashauri na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Babati.

Kwa upande wake Mganga Mkuu Halmashauri ya Mji wa Babati Bw. Nasibu Msuya amesema watahakikisha wanasimamia huduma bora hospitalini hapo na kuondoa malalamiko kwa wateja na wameanzisha kundi sogozi kwa ajili ya kuwapa fursa wananchi kutoa maoni na malalamiko yao kupitia kundi hilo.

Nae Mwenyekiti wa kamati hiyo Bw. Peter Sulle amepongeza Halmashauri ya Mji wa Babati kwa kusimamia vyema mradi huo na kukamilika kwa wakati.

Nao Wajumbe wa kamati hiyo Bi. Rose Kamili na Bi.Benadetha Tsere wakiwa kwenye Hospitali hiyo ya Mji Babati (Mrara) wamefurahishwa na utekelezaji wa ujenzi huo na kutaka huduma zitakazo tolewa kuwa bora zaidi kwa kujali wanao hudumiwa ili kuondoa malalamiko.

Nishati Safi ya kupikia yarahisisha zoezi la uchomaji Nyama
Wabunge Massay, Regina wawagusa Wazazi Manyara