Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, Marco Rubio na Mshauri wa Usalama wa Taifa, Mike Waltz kwa pamoja Machi 11, 2025 wanatarajiwa kuwa Saudi Arabia, ili kufanya mazungumzo na Viongozi wenza wa Ukraine.
Hatua hiyo, inakuja baada ya Rais wa Taifa hilo, Donald Trump kusema uongozi wa Ukraine uko tayari kuendelea na pendekezo la Marekani la kuanzisha mchakato wa kusitisha mapigano na Urusi.
Trump ameongeza shinikizo kwa rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky kumkubalia ombi lake la kusitisha mapigano na Urusi, bila ya uwepo wa ahadi ya dhamana ya usalama kutoka Marekani.
Hivi karibuni, wawili hao walipishana kauli hadharani wakiwa Ikulu ya White House, ambapo Trump alidai kuwa Zelensky hakuwa tayari kumaliza mapigano, huku kiuhalisia Moscow ikiwa inadhibiti takribani asilimia 20 ya ardhi ya Ukraine.