Saulo Steven – Karatu.
Washiriki wa kozi ya waalimu wa mpira wa miguu ngazi ya awali Grassroots wametakiwa kuitumia vizuri nafasi waliyoipata kwa kwenda kuwafundisha na kuupenda mpira wa miguu watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 6-12.
Akizungumza Wilayani Karatu wakati wa ufunguzi wa kozi hiyo ya siku tano Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Karatu Juma Musa Hokororo amesema lengo kubwa la kuanda mafunzo hayo ni kuwapa ujuzi walimu ambao watakwenda kusaidia kufumbua na kuviendeleza vipaji vya watoto.
Kwa upande wake Mkufunzi wa Kozi ya Grassroots Raymond Gweba akizungumzia katika ufunguzi wa wa kozi hiyo amempongeza Mkurugenzi kwa kuandaa kozi hiyo na kuwaomba washiriki wa mafunzo hayo kutilia maanani kile wanachofundishwa kwani mafunzo hayo ndio msingi wa kuwa mwalimu wa mpira wa miguu.
Kalisti Kipalazya na Asnati Ndosi ni miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo wamesema yatakwenda kuwasaidia katika kukuza vipaji vya watoto mashuleni,ikumbukwe mafunzo hayo yatadumu kwa siku tano kuanzia tarehe 10/3/2025 hadi 15/3/2025 yenye jumla ya washirki Zaidi ya 35 kutoka wilayani Karatu.