Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeshiriki kikamilifu katika kutoa maoni katika utengenezaji na uandaaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 ili kuhakikisha kuwa Dira hiyo inaakisi masuala yote ya Sekta ya Sheria.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari amezungumza hayo katika mahojiano maalumu na Vyombo vya Habari yaliyofanyika Ofisini kwake, Mtumba Jijini Dodoma, Machi 10, 2025.
Amesema, Ofisi yake imejipanga kuhakikisha kwamba mambo yote yanayoihusu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yanatekelezwa ipasavyo ili kuweza kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2050.
“Sisi kama Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali tutahakikisha kwamba tunaoanisha vizuri Sheria zetu tulizonazo na kule tunakotaka kwenda, ni lazima tuwe na legal framework ya kutufikisha,” amesema.
Aidha, amesisitiza suala la kufanya maboresho katika Sheria mbalimbali ziweze kuendana na mabadiliko ya Kijamii, Kiuchumi pamoja na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa Sheria.
“Sisi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali tunataka kuwa champion wa kuhakikisha kuwa sheria zetu zote tunazioanisha na Dira ya Taifa ya 2050.” amesema Johari.
Katika hatua nyingine Mwanasheria Mkuu huyo wa Serikali ameongelea suala la ufasiri wa Sheria, ambapo amasema kwakua Sheria mbalimbali zimeweza kutasfiriwa kutoka lugha ya Kingereza kwenda Kiswahili kwakuwa ili ziweze kutumika kwa urahisi na watumiaji