Johansen Buberwa – Kagera.

Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCN (UVCCM) mkoa Kagera imeanzisha Kampeni ya siku 16 yenye lengo la kutafuta wapiga kura wapya wa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na Vijana katika maeneo mbali mbali kwenye ziara hiyo iliyoanza wilaya karagwe Machi 11, 2025 Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera, Faris Buruhan amesema ziara hiyo iliyopewa jina la Samia New Voters Campaign (SANEVO).

Amesema, “Vijana wa Wilaya ya Karagwe mnayo sababu kubwa ya kutembea kifua mbele na kujivunia kuwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amehakikisha miradi mikubwa ya maendeleo inakuja katika jimbo la Karagwe kwa kushirikiana na mbunge wenu ambaye ni Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa.”

Awali Katibu wa Jumuiya yaUmoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa huo, Christina Hussein aliwaomba Vijana wote Mkoa Kagera kumpigia kura Dkt. Samia ili aweze kuwa Rais wa Tanzania, huku Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Karagwe, Alex Jacob akiihakikishia kamati hiyo kuwa Vijana wote wanamchagua Dk Samia kwasababu ya uchapa kazi wake na jinsi alivyounganisha vijana wote nchini kwenye suala la ajira na uchumi.

Pinda arejesha matumaini kwa Wasioona, wenye tezi dume Kavuu
Wananchi wanaendelea kupata Maji kwa uhakika - Mha. Bwire