Usiku wa Machi 12 2025, Clouds Media Group imezindua msimu mpya wa Malkia wa Nguvu 2025 Jijini Dar es salaam wenye kauli mbiu ya TWENDE DUNIANI, ambao kwenye uzinduzi huo imetangazwa kuwa Malkia wa Nguvu mwaka 2025 itafika kwenye Kanda tano za Nchi ya Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amesema kuwa azma na maono yake kwa miaka 30 iliyopita ni kuwa na jukwaa la Wanawake tu ambalo kwa sasa imewezekana japo mwanzo watu wengi hawakumuelewa na kumuamini.

‘Azma na maono yangu kwa miaka 30 iliyopita ni kuwa na jukwaa ambalo Wanawake watahusika kwenye kila kitu ninachokifanya, Hizi tuzo za Malkia wa Nguvu wazo lake lilianzia kwenye Mwanamke Mjariamali aitwae Mwanamakuka sisi tuliona hili wazo tulifanye kwa ukubwa na ndio hiki tunakisherehekea leo’ – Kusaga.

Joseph Kusaga ameongeza kwa kusema ‘Tumeanzisha Redio mpya ya Wanawake tu iitwayo Malkia Choice FM, Hii ni sauti ya Wanawake, sisi tunaamini Wanawake ninyi ni bora sana Duniani, na siku ya tarehe 04/04/2025 tunamualika Mhe. Rais Samia najua anatusikiliza Watoto wake, siku hiyo iwe siku kubwa tusherehekee nae Rais wetu kwenye hii siku kubwa ya Malkia wa Nguvu Dar’ – Kusaga.

Clouds Media Group imesema kuwa TUZO ZA MALKIA WA NGUVU 2025, zitapita kwenye Kanda ya ziwa, Kanda ya Kati, Nyanda za Juu kusini, Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Pwani.

SEforALL kuimarisha ushirikiano upatikanaji Nishati endelevu
Serikali kuendeleza mikakati ukuzaji Sekta ya Mifugo