Jeshi la kujenga Taifa (JKT), limesema lipo tayari kutoa ushirikiano kwa Taasisi mbalimbali za ajira, ili kuwachukulia hatua kali Vijana wanaogushi vyeti vya jeshi hilo na kuvitumia kuajiriwa kwenye taasisi na Makampuni yanayohitaji watendaji waliopitia JKT.
Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Makao Makuu ya Jeshi hilo Chamwino Mkoani Dodoma, Kanali Juma Mrai ameyasema hayo wakati akizungumza na Wanahabari.

Amesema, “Jeshi la kujenga Taifa linautaarifu UMMA wa watanzania kwa wale wote waliobainika na watakao bainika kugushi cheti cha kujenga Taifa kwa matumizi yoyote yale, hatua kali za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao.”
“Jeshi la kujenga Taifa lipo tayari kutoa ushirikiano kwa taasisi na makampuni yote yanayohitaji uhakiki wa vyeti vya kujenga Taifa kwa watumishi wao waliopitia mafunzo ya kujenga Taifa,” aliongeza Kanali Juma Mrai.