Johansen Buberwa – Kagera.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi – UVCCM, Mkoa wa Kagera, Faris Buruhani amewataka Vijana kujitokeza na kushiriki uchaguzi Mkuu ujao kwa kupiga kura na kugombea nafasi mbalimbali.

Buruhan aliyasema hayo mara baada ya kukishukuru kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Taifa, kuja na kauli mbiu ya ‘kazi na utu tunasonga mbele kwa Mwaka 2025-2030.

Faris alitoa pongezi hizo katika kikao cha baraza la UVCCM Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera Katika ukumbi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilayani humo akiwa katika ziara ya siku 16 ya kutafuta wapiga kura wapya wa Dkt. Samia Suluhu Hassani na kuzitafuta kura za Chama Cha Mapinduzi za Wabunge na Madiwani.

“Nawapongeza wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa walioketi march kumi mwaka Huu kwa kupitisha kaulimbiu mpya ambayo itatumika 2025 Mpaka 2030 ikiwa ni Kauli mbiu mpya ambayo italeta maendeleo makubwa kwa wananchi na watanzania kwa ujmla,” alisema Buruhan.

Hakuna ugonjwa wa Marburg tena Tanzania - Serikali
Dkt. Buriani awaita wadau kuwekeza kituo cha Sayansi Stem Park