Baridi yabisi.
Baridi yabisi ni moja ya magonjwa kwenye kundi la (autoimmune diseases) magonjwa yanayotokana na kinga ya mwili kushambulia tishu za mwili na kupekelea tishu hizi kututumka na kuvimba.
Tatizo hili huathiri maeneo ya maungo na kuletekeza maumivu makali yasiyokwisha, kuvimba kwa joint na kusababisha ugumu kukunja viungo. Tatizo linaweza kuwa kubwa pale mpambano kwenye joint (inflammation) unapokuwa mkubwa na baadaye maumivu hupungua.
Kwa mgonjwa mwenye baridi yabisi ni muhimu kurekebisha lishe na mtindo wa maisha kama ambavyo nitaelekeza hapa chini ili kupunguza makali ya ugonjwa.
Ugonjwa wa baridi yabisi kama usipochukuliwa hatua za haraka kuudhibiti unaweza kusababisha matatizo makubwa kama kuharibika kwa maungio, neva na athari kwenye mishipa ya damu.
Baridi yabisi husababishwa na muunganiko wa sababu ikiwemo lishe, vinasaba, mtindo wa maisha, vichocheo pamoja na kinga ya mwili.
Tafiti zinasema kwamba kwa mgonjwa anayeanza tiba mapema hupata nafuu zaidi na kuepuka madhara ya baridi yabisi.
Pamoja na dawa za hospitali wataalamu wa tiba asili tunashauri mgonjwa azingatie zaidi lishe na mazoezi ili kupunguza maumivu.
Dalili.
Dalili za Baridi yabisi hutokana na kupotea kwa utando mweupe uliopo mwishoni mwa mfupa (cartilage) ambao hupunguza msuguano kati ya mfupa na mafua, kuvimba kwa tishu zinazozunguka jointi na kukaza kwa joint.
- Kwa mgonjwa mwenye baridi yabisi ute uliopo kati ya mfupa na mfupa hupungua na kufanya mifupa kusagana. Dalili kuu za mgonjwa mwenye baridi yabisi ni :-
- Maumivu ya joint
- Kuvimba kwa tishu zinazozunguka maungio ya mifupa husababisha maumivu makali kwa mgonjwa.
- Jointi zinazoathirika zaidi ni kwenye mikono, enka, vidole vya miguuni na kwenye magoti.
- Ngozi ya joints kuwa nyekundu, laini na inayochoma kama vile imeungua moto.
- Maumivu na kushindwa kusonga mbele baada ya kuamka asubuhi, hali hii huchukua dakika 30 na baaade mgonjwa anaweza kuendelea kutembea.
- Mwili kufa ganzi na maumivu ya misuli.
- Kupata ugumu kwenye kutembea, kushika kitu, kufanya mazoezi na kupanda ngazi.
- Kwa baadhi ya wagonjwa hupoteza hamu ya kula na kupata homa za muda mfupi.
Madhara.
Kwa baadhi ya wagonjwa wenye baridi yabisi hupata madhara ya kiafya ya muda mrefu mwilini.
Tafiti zimebaini matatizo haya huzaliwa na uwepo wa arthritis.
- Kuongezeka kwa hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kiharusi.
- Maumivu ya kifua, pumzi kukata na kushindwa kupumua kutokana na athari kwenye mapafu.
- Maumivu ya kichwa yasiyoisha.
- Matatizo ya figo na kujikusanya kwa maji mwilini.
- Maumivu na kudhoofika kwa mifupa
- Kuishiwa damu na kupata ganzi.
- Kuota vinyama vidogo vidogo kuzunguka eneo la maungio ambavyo huongeza ukali wa maumivu.
Tiba.
Madaktari hutibu maambukizi yaliyosababisha ugonjwa wa baridi yabisi ikiwa hayajakwisha.
Madaktari wanaweza kupendekeza dawa za kusaidia kupunguza maumivu ya viungo na dalili zingine, ikiwa ni pamoja na:
-
Dawa za kupunguza uvimbe zisizo na steroidi (NSAID), ili kupunguza maumivu na kuvimba kwa viungo
-
Sindano za kotikosteroidi kwenye viungo vilivyofura
-
Wakati mwingine, dawa zinazodhibiti mfumo wa kinga mwili, ili kupunguza uvimbe.
Tiba ya mazoezi ya mwili inaweza kusaidia kulegeza viungo na matatizo ya macho na ngozi yanayotokana na ugonjwa wa baridi yabisi uliosababishwa na maambukizi katika sehemu nyingine ya mwili hayahitaji kutibiwa.