Boniface Gideon – Tanga.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imelipongeza Shirika la Reli Nchini – TRC, kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa Reli ya Kisasa ‘SGR’, Pamoja na maboresho ya Miundombinu ya Shirika hilo huku Kamati hiyo ikiitaka Mamlaka ya Bandari Nchini ‘TPA’ pamoja na shirika la Reli ‘TRC’ kuanza kutekeleza mpango wake wa kuunganjisha njia ya Reli na Bandari ya Tanga ambapo kukamilika kwake linatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa ndani na nje ya nchi.

Maagizo hayo yametolewa na Mwenyekiti wake Suleiman Kakoso, wakati walipofanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya upanuzi wa bandari , uwanja wa ndege pamoja na maboresho ya Reli iliyopo Mkoani hapa ambapo wameipongeza Serikali kupitia maboresho yanayofanyika katika miradi hiyo.

“Tumefurahishwa na mipango ya baadaye ambayo sasa mamlaka ya bandari nafikiria kwenda mbali zaidi muanze kuweka mifumo ya kuunganjisha Reli na Bandari ili tuwe na miradi mikubwa,” alisema.

Aidha, ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya ujenzi na uchukuzi ambayo imeanza michakato ya ujenzi wa Reli za Kisasa katika maeneo mbalimbali nchini ambayo utakapo kamilika itafungua fursa mbalimbali ikiwemo za kiuchumi.

“Kitendo cha kuanza kufikiria kujenga Reli za Kisasa Mikoani itasaidia sana kuongeza mzunguko wa fedha kwa Wananchi wetu,tunashauri Serikali iwe inashirikisha wawekezaji katika ujenzi wake” alisema Kakoso

“Pamoja na uwekezaji mkubwa ambao mnaweka kwenye kwenye Shirika la Reli,Bunge linashauri ni vyema uwekezaji wenu uende sawa na vitendea kazi ili uwekezaji uwe na tija” alisema.

Alisema mkoa wa Tanga unaendelea kufunguka kupitia fursa mbalimbali ikiwemo za kiuchumi katika utekelezaji wa miradi mikubwa kama ujenzi wa Barabara, ukarabati wa Reli samabama na ujenzi wa Barabara ya Tanga hadi Singida pamoja na Ile ya Tanga hadi Bagamoyo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi uendeshaji kutoka shirika la Reli Tanzania ‘TRC’ Focus Sahani ameeleza kuwa wameendelea kuhakikisha usafiri wa njia hiyo unaimarika ambapo hadi kufikia sasa Kila wiki wa siku nne wanayoa huduma ya safari za Treni za abiria kutoka Dar es salaam,Korogwe Moshi na Arusha.

“Tumepata pongezi kubwa sana kuhusu uanzishwaji wa Treni ya kisasa ya SGR pamoja hiyo lakini tuna Treni yetu ya MGR tunatoa huduma ya Tren ya abiria katika mikoa ya Kanda ya kaskazini Kila wiki tuna safari nne za Treni tangu tulipoifungua hiyo Reli, Kila tunapofika kuanzia mwezi November mpaka February huwa tunaong za Treni zinakuwa sita kwa wiki kwaajili ya kuwahudumia watanzania” alisema Sahani.

Alisema Shirika linaendelea na kazi ya kuzifungua Reli zinazoelekea katika bandari ya Tanga ambapo kazi iliyopo ni kubadilisha miundombinu iliyopo kutokana na uchakavu wake ambapo Serikali imetoa fedha kwaajili ya ujenzi huo.

“Kwa hapa Tanga bado tunaendelea kufungua hizo Reli kwaajili ya kwenda bandarini kilichobakia sasa ni kuboresha njia za Reli karibu na eneo la bahari juhudi zinaendelea kufanyiwa kwa sababu Reli hizo zimechakaa na Serikali sasa imeshayoa fedha kwaajili ya kupata vifaa vya ujenzi huo”

Akizungumzia juu maendeleo ya mradi wa Reli ya kisasa ‘SGR’ Sahani amesema kuwa baada ya kukamilika kwake na kufanyiwa majaribio na hatimaye kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan tayari mpaka zipo Treni 8 za abiria zinazotoa huduma ya safari za abiria kutoka Dar es salaam hadi Dodoma.

” TRC baada ya kupewa mamlaka ya kusimamia Reli tulianza na ujenzi ya SGR’ kilichofuata ni uendeshaji wa Tren ambapo tulianza kwenye majaribio kuanzia Dar es salaam kwenda Morogoro, lengo likiwa ni kufika Dodoma baadaye tulianza majaribio ya kwenda Dodoma tukaanza oparesheni na mpaka sasa tuna safari 8 za Treni kwenda Dodoma maana yake Dar es salaam na Dodoma sasa hivi imekuwa ni karibu,” alisema.

Kanuni Ujenzi wa Majengo kuondosha kero nyingi
Diaspora waahidiwa ushirikiano uchangamkiaji fusra za kiuchumi Nchini