Rais wa Urusi, Vladmir Putin amesema anakubaliana na wazo la kusitisha vita nchini Ukraine kwa siku 30, lakini kwa kutoa masharti yaliyompa mashaka Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky.
Katika kauli yake, Putin amesema mkataba wowote wa usitishwaji vita ni lazima ulete amani ya kudumu na kutatua changamoto za msingi za mzozo huo.
Ameongeza kuwa, moja ya sharti ambalo litamfanya kukubali kusitisha mapigano hayo kwa muda uliopendekezwa ni kulitambua jimbo linalowania la kursk kuwa lipo upande wa Urusi.