Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni ya Mkoani Kigoma, imekanusha Picha mjongeo iliyonakilishwa na Mange Kimambi Machi 13, 2025 kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Kijamii wa X, juu ya uwepo wa mgonjwa wa Mpox.

Kupitia taarifa iliyotolewa hii leo Machi 14, 2025 na Uongozi wa Hospitali hiyo ya Maweni RRH, imeeleza kuwa video hiyo iliyochapishwa ni ya Septemba, 2024 ni ya mgonjwa aliyetambuliwa kuwa ni Issa Omary Ndadhitezima.

“Kijana anaonekana amejirekodi video fupi katika chumba cha Hospitali ambacho tumekitambua kama ni moja ya vyumba vya Hospitali yetu ya Maweni_ Uongozi wa Hospitali unapenda kutoa taarifa kwa Umma ya kwamba “video” hiyo iliyochapishwa siyo ya sasa bali ni ya zamani (Septemba, 2024),” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, “Mgonjwa huyo tuliyemtambua kama Issa Omary Ndadhitezima alilazwa akiwa mshukiwa wa ugonjwa huo wa mlipuko, lakini hata hivyo, baada ya vipimo vya maabara iligundulika kwamba hana maambukizi ya Mpox. Hivyo mgonjwa huyu alitibiwa kama mgonjwa wa kawaida wa shida ya ngozi na kisha kuruhusiwa.”

Kufuatia hali hiyo, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma, imeutaarifu Umma kuwa kwasasa hatuna mgonjwa yeyote wa Mpox aliyelazwa na kwamba imejiandaa kukabiliana na aina yoyote ya magonjwa ya mlipuko.

“Uongozi wa Hospital’ ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma unapenda kutoa rai kwa Umma kuacha kutoa au kusambaza taarifa hii kwani haina ukweli na inazua taharuki bila sababu,” ilimalizia sehemu ya taarifa hiyo.

LEONBET Inakuletea 1000% Boost Kwenye Mikeka Yako
Putin atoa masharti ili kusitisha mapigano kwa siku 30