Baraza la Vyama vya Siasa nchini limekemea vikali upotoshaji wa wadau wenzao, kikiwemo Chama cha ACT Wazalendo kilichochapisha vipeperushi vya kubagaza Baraza hilo kama njia ya kuharibu utendaji kazi wake licha ya kuanzishwa kwa minajili ya kujenga umoja na mazingira mazuri ya kisiasa hapa nchini.

Hayo yameelezwa na wajumbe wa baraza hilo wakati wa kikao cha kawaida hilo lililofanyika kwa siku mbili, Machi 12 na 13 mwaka huu mkoani Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu mkuu wa chama cha National League For Democracy (NLD) Doyo Hassan Doyo amesema kuwa Baraza hilo ni chombo kilichundwa kishereia kupitia Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo halistahili kudharauliwa na wadau wa siasa, vikiwemo vyama vya upinzani nchini hapa.

“Juzi tumeona taarifa ya chama cha ACT WAZALENDO kuwa hawatashiriki baraza la vyama vya siasa kwa kwa madai baraza halifanyi kazi zake vya kuviwezesha vyama vya siasa na kutunza demokrasia nchini, kitu ambacho sio kweli,” alisema Doyo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa chama cha Democratic Party DP ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya siasa na Bunge Abdul Mluya amesema baraza lao ni kiunganishi kikubwa kati ya vyama vya siasa na serikali.

“Ukiona watu wanatusi chombo ambacho hata kiongozi wao mkuu amenufaika nacho na kumpa heshima kubwa jua chama hicho hakijui kinataka nini zaidi ya kuanzisha vurugu na chokochoko tu,”Amesema Mluya.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 14, 2025
Hakuna ugonjwa wa Marburg tena Tanzania - Serikali