Boniface Gideon – Morogoro.

Mwanasiasa na kada wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo ametangaza rasmi azma yake ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao kupitia Chama hicho,huku akina na Agenda 10 z Taifa.

Doyo, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama hicho,ametoa tangazo hilo mwishoni mwa wiki, mbele ya waandishi wa habari jana mkoani Morogoro na kuwataka Wananchi kumuunga mkono ili atimize lengo la kuwatumikia Wananchi katika nafasi hiyo ya ngazi ya juu zaidi ya Utawala hapa Nchini.

Doyo aliwashukuru Watanzania kwa mwitikio wao wa kuendelea kukuza demokrasia nchini, akisisitiza kuwa ni muhimu kwa kila Mtanzania mwenye sifa kupata haki ya kuchagua au kuchaguliwa.

“Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, ambapo kila Mtanzania mwenye sifa anayo haki ya kuchagua na kuchaguliwa,” alisema.

Doyo aliongeza kuwa, yeye mwenyewe ana sifa zote zinazohitajika kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisisitiza kuwa amevuka umri wa miaka 45, umri wa kikatiba wa kugombea nafasi ya urais, na kwamba ana afya ya kuhimili majukumu ya nafasi hiyo.

Akizungumzia umuhimu wa uchaguzi mkuu ujao, Doyo alisisitiza kuwa huu utakuwa uchaguzi wa sita tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini, na kwamba ni muhimu kwa maendeleo ya taifa. “Kama Mtanzania mwenye haki ya kikatiba, nimemudu kujitathmini kifikra, kiuwezo, na kiuweledi, na kujiridhisha kuwa nina uwezo wa kumudu nafasi hii,” alisema Doyo.

Doyo alifafanua kuwa uamuzi wake wa kugombea urais haujaanza kwa mkupuo, bali ni baada ya kupata busara kutoka kwa wazee na familia yake, ambao walimshauri kuendelea mbele kwa faida ya taifa.

“Si busara kuwataja hapa, lakini wanajua na wanasikia wakiwa pale walipo,” alieleza.

Amesema amekuja na Agenda 10 ambazo anaona bado hazijapata kipaumbele kikubwa katika Taifa na kwamba ataenda iwapo atachaguliwa kuwa Rais ataenda kuyashughulikia.

“Kuna mambo ambayo naona hayajakaa sawa katika Taifa letu,na endapo nitachaguliwa kuwa Rais nitaanza nayo, hivyo Agenda zangu Kuu ni ajira, elimu, kilimo na ufugaji, rasilimali za maji, kupambana na ukwepaji wa kodi, na kupambana na rushwa, kuimarisha sekta ya madini, kuimarisha muungano, na kuendeleza jitihada za watoto wa kike katika elimu na teknolojia.

“Kwa hiyo, nimeona ni muhimu kutoa mchango wangu kwa Taifa letu ili kuleta faraja kwa Watanzania. Hivyo, leo hapa mbele yenu, mimi Doyo Hassan Doyo, mwanachama wa Chama cha National League for Democracy (NLD), natangaza nia ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama chetu cha NLD.

Dhamira yangu ni kubeba dhana ya Uzalendo, haki, na maendeleo kwa vitendo ili tuwakomboe Watanzania,” alisisitiza Doyo.

Maisha: Nilifanya hivi kuipata Bodaboda yangu iliyoibiwa