Serikali imetoa fedha na kuweka mazingira rafiki kwa wanasayansi na wabunifu wa Kitanzania Kupitia mfumo wa ushirikiano wa kimkakati kati ya serikali ya Tanzania na nchi rafiki pamoja na taasisi za kimataifa.

Akizungumza hayo na Waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu, leo Machi 17,2025 Jijini Dodoma, ambapo amesema COSTECH imepokea shilingi bilioni 5.65 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya utafiti wa pamoja kati ya watafiti wa Tanzania na washirika wao.

“Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, serikali imetenga shilingi bilioni 6.3kwa ajili ya miradi ya utafiti wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, huku shilingi milioni 600 zikielekezwa katika miradi minne ya usalama wa chakula, ikihusisha udhibiti wa magonjwa ya mazao, uboreshaji wa uhifadhi wa chakula na ubunifu wa vyakula vyenye virutubishi vya hali ya juu”,amesema

“COSTECH imeanzisha na kuziwezesha kongano nane bunifu katika mikoa ya Kigoma, Geita, Mafia, Mbeya, Dodoma, Morogoro, Singida na Pemba ili kusaidia sekta ya viwanda na kilimo, Miradi hii imewezeshwa kwa ufadhili wa shilingi milioni 750, kuhakikisha teknolojia bora zinatumika katika kuboresha uzalishaji wa mafuta ya mawese, dhahabu na mazao ya baharini”. Amesema Dkt. Nungu.

Vilevile amesema Kwa kuwekeza shilingi bilioni 2.3 kupitia Samia Commercialization Fund, serikali imewapa wabunifu wa Kitanzania fursa ya kuingiza bunifu zao sokoni, hii inasaidia kuondoa changamoto ya kukosekana dhamana ili kupata mitaji.

Hata hivyo amesema COSTECH imefanikiwa kuandaa mifumo ya usimamizi wa tafiti kwa kutumia teknolojia za kidijitali kupitia mradi wa HEET, pamoja na kuanzisha vigoda vya utafiti katika vyuo vikuu kama SUA na NM-AIST kwa ufadhili wa shilingi bilioni 4.7

“Kwa mafanikio haya, Tanzania inajiweka katika nafasi ya ushindani wa kimataifa katika nyanja ya sayansi na teknolojia, na uwekezaji huu si wa kawaida, bali ni hatua ya kimkakati inayoonesha kuwa Rais, Dkt. Samia Suluhu ameleta mapinduzi katika sekta ya sayansi na teknolojia, ikiwa ni kielelezo cha uongozi wenye dira na maono makubwa kwa taifa”, amesema

“Katika kuimarisha miundominu ya utafiti, pamoja na kutoa fedha kwa vyuo vikuu, Serikali imetoa TZS 9 bilion kuhakikisha kuwa jengo la COSTECH linafanyiwa ukarabati na pia tunajenga jengo jipya hapa Dodoma”. Amesema Dkt. Nungu.

Tunatambua umuhimu wa Maji katika kukuza uchumi
Kima cha chini Pensheni ya kila mwezi kimeboreshwa - Mshomba