Wilaya ya Mlele imefanya hafla ya kupongeza miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Ibelamafipa iliyopo Kijiji cha Ilunde Halmashauri ya Mlele mkoani Katavi.
Katika maadhimisho hayo Sungusungu wa Mlele wameonekana kuwa kivutio kikubwa wakati wa maandamano ambao walionesha hisia zao za shukrani kwa kuingia na nyimbo zao za asili.
Wakizungumza viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya hiyo Alhaj Majid Mwanga pamoja na wakurugenzi wake kutoka Halmshauri ya Mlele na Mpimbwe wameelezea walivyopokea zaidi ya shilingi bilioni 507 kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa rais Samia Suluhu Hassan na kutumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Elimu, afya, miundombinu ya barabara, umeme na maji.