Mbio za Bunge Marathon zinatarajia kufanyika Aprili 12, 2025 jijini Dodoma ambapo fedha zitakazokusanywa zitatumika kujenga Shule ya Sekondari ya wavulana katika eneo la Kikombo Jijini Dodoma.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Maandalizi ya mbio hizo, Festo Sanga amesema mbio hizo ambazo zinaandaliwa kwa mara ya pili, zinatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 5,000 na zitakuwa za nusu marathon yaani kilomita 21, kilomita 10 na kilomita 5.
Amesema, ada ya ushiriki wa mbio hizo ni shilingi 40,000/- ambayo mshiriki atapatiwa Marathon Kit itakayojumuisha fulana, mfuko na namba ya kukimbilia.

Amesema mbio hizo ni za watanzania wote wa ndani na nje ya Tanzania na kuwakaribisha kushiriki katika ajenda muhimu ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavula.
“Bunge la Tanzania limeshajenga Shule ya Sekondari ya Wasichana katika eneo la Kikombo, jijini Dodoma na sasa hivi tunashirikiana na watanzania kupitia Mbio hizi kujuenga Shule ya Sekondari ya Wavulana jijini Dodoma. Hivyo nawaomba watanzania mjitopkeze kwa wingi kushiriki katika mbio hizi.
“Mchango wa mbio za marathon utasaidia sekta ya elimu utaongozwa na Waheshimiwa Wabunge huku ikiambatana na dhamira ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukuza michezo na elimu, mbio hizi pia zinatoa fursa kwa Wabunge kuimarisha uhusiano wao na Watanzania sambamba na kuendeleza utimamu wa mwili na kuishi kiafya.” Amesema.

Akizungumzia washindi, Sanga amesema kwenye nusu marathon yaani kilometa 21, mshindi wa kwanza atajinyakulia Milioni 5, mshindi wa pili atapata Milioni 3 na mshindi wa tatu akiambulia Milioni 1.5.
Kwa upande wa kilomita 10, mshindi wa kwanza atazawadiwa shilingi milioni 2, mshindi wa pili Shilingi 1.5, na mshindi wa tatu atajinyakulia shilingi milioni moja huku. Katika kilomita 5 mshindi wa kwanza atapata shilingi 1.5, nafasi ya pili akipata milioni moja na mshindi wa tatu atapata shilingi laki tano.
Kwa upande wake Mkuu wa GSM Foundation, Faith Gugu amesema Bunge Marathon imebeba Agenda zao zote ambazo ni afya michezo na elimu ndio maana wakashawishika kudhamini mbio hizo.

“Tumevutiwa na lengo la hizi mbio ndio maana tumedhamini, tunaunga mkono mambo mengi na bunge Marathon ambayo imebeba ajenda zetu zote na utadhamini vifaa vyote vya mbio hizo pamoja na maji” alisema
Naye, Meneja NHIF Mkoa wa Ilala, Dkt. Aifena Mramba amesema mfuko umeunga mkono mbio hizo kwa sababu zitakuwa na manufaa kwenye jamii ya Watanzania kusaidia kujenga afya.
“NHIF tumeona ni muhimu kuunga mkono mbio hizi kwa sababu zitakuwa na manufaa ya kujenga afya za wateja wetu ambao ni watanzania kwa ujumla wao na Shule ni washirika wetu ndio maana tumedhamini maana wanafunzi wengi ni wanachama wetu, suala hili litaingia kwenye idara zetu zote na wafanyakazi wetu watashiriki mbio hizi” alisema.