Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limetoa ufafanuzi wa taarifa inayosambaa katika Mitandao na picha mjongeo, ikimuonesha Mkazi jiji hilo, Mercy Daniel akielezea tukio la kupotea kwa mumewe David Gipson na kuda kuwa wao hawajamshika mtu huto.

Taarifa iliyotolewa hii leo Machi 18, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Justine Masejo imesema Jeshi hilo limepokea taarifa hiyo na uchunguzi wa shauri hilo unaendelea.

Amesema, katika ufuatiliaji uchunguzi wa awali umebaini kuwa David Gipson amehusishwa na upotevu wa fedha uliotokea katika benki moja jijini Arusha na kwamba Polisi wanaendelea na ufuatiliaji wa shauri hilo, ili kubaini alipo mtu huyo na taarifa kamili itatolewa.

Maeneo ya kijamii yamepewa kipaumbele kufikiwa na Umeme - Kapinga
TBS yatenga Bilioni 2.7 kuimarisha ofisi za kikanda