Naibu Waziri Nishati, Judith Kapinga amesema utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini umetoa kipaumbele kwenye maeneo yanayotoa huduma za kijamii ikiwemo Shule, Taasisi, vituo vya afya, zahanati na maeneo ya visima vya maji kwa sababu ni maeneo yanayotoa huduma kwa jamii

Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Machi 18, 2025 katika Vijiji vya Lwangu na Welela vilivyopo katika Halmashauri ya Njombe wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kukagua miradi ya umeme vijijini pamoja na kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo.

“Kipaumbele ni Taasisi kwa sababu zinatoa huduma zinazotunufaisha sisi wote, tunataka umeme ukatumike kwenye vituo vya afya, zahanati, kwenye visima vya maji lakini pia kwenye shule”. Amesema Mhe. Kapinga.

Ameongeza kuwa, kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini hufanyika tathmini ili kuyabaini maeneo yanayotoa huduma za kijamii huku akibainisha hakuna maeneo yanayo rukwa.

Njombe: Wananchi waiomba TANESCO, REA kuongeza kasi ya kuwaunganishia Umeme
Tunamtafuta Gipson, tutatoa taarifa kamili - Polisi Arusha