Mimba za utotoni ni ujauzito anaoupata Mwanamke aliye chini ya umri usiofaa katika jamii fulani, ambazo zinahusishwa na masuala ya kijamii, ikiwa ni pamoja na viwango vya chini vya elimu na umaskini.

Tatizo hili la mimba za utotoni limekuwa kubwa duniani na linaongezeka siku hadi siku hasa katika jamii ya uchumi wa chini huku sababu zinazopelekea jamii ya uchumi wa chini kukumbwa sana na tatizo hilo ni ukosefu wa taarifa za afya ya uzazi na umasikini.

Tanzania inaendelea na mapambano dhidi ya mimba za utotoni, ingawa bado kuna changamoto, tukikumbuka kwamba Oktoba 28, 2023 wakati akizungumza katika uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na viashiria vya Malaria Rais Samia mikoa inayoongoza mimba za utotoni ni Songwe asilimia 45, Ruvuma asilimia 37, Katavi asilimia 34, Mara asilimia 31 na Rukwa asilimia 30.

Ripoti ile ilionesha kumekuwa na mafanikio katika kupunguza mimba za utotoni kwa asilimia 5 kutoka asilimia 27 mwaka 2015/2016 hadi asilimia 22 mwaka 2022 lakini tukilitizama tatizo hili kwa upande wa pili mbali na umasikini ama hali ya kiuchumi ni wazi kuna mporomoko pia wa maadili.

Wafanyabiashara wa Mbolea waliopewa leseni wafikia 7,302
Maisha: Atupiwa gonjwa kishirikina, usaidizi wa Kiwanga wamuokoa