Benki ya Maendeleo TIB imeripoti kuwekeza zaidi ya Shilingi bilioni 630.3 katika miradi ya maendeleo hadi kufikia Desemba 2024.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Lilian Mbassy amesema Kati ya kiasi hicho, Shilingi bilioni 408.3 zipo kwenye mizania ya Benki, huku mifuko tisa inayosimamiwa na Benki ikichangia uwekezaji wa Shilingi bilioni 222.

“Uwekezaji huu ni wamiradi ya muda wa miaka 5-15 katika sekta mbalimbali za maendeleo. kupitia uwekezaji huo mkubwa zaidi ya ajira mpya 12,547 zimezalishwa kutokana na Benki kufadhili miradi ya muda mrefu nchini,” amesema.

Mbassy ameongeza kuwa, uwekezaji huu umegusa maeneo ya kipaumbele ya Serikali pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) hasa katika Shilingi 162.7 bilioni zimewekezwa kuongeza usalama wa chakula na kupunguza njaa.

“Shilingi 4.3 bilioni zimewekezwa
kuboresha elimu kupitia miradi ya taasisi za elimu, Shilingi 22.4 bilioni zimewekezwa
katika upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazingira kupitia miradi ya mamlaka za maji.

Uwekezaji mwengine ni Shilingi 11.5 bilioni zimewekezwa katika nishati safi na nafuu
kupitia mradi wa upanuzi wa nishati ya umeme vijijini (Tanzania Rural Electrification Expansion Programme-TREEP).

“Shilingi 250.7 bilioni zimewekezwa katika ukuaji wa uchumi na ajira, ikihusisha sekta za utalii, viwanda, na usafirishaji na Shilingi 24.7 bilioni zimewekezwa kuboresha miji na makazi”. Amesema Mbassy

Hata hivyo amesema Benki itaendelea kukuza mtaji wa Benki kwa kushirikiana na taasisi za fedha za kimataifa ili kupata mikopo ya riba nafuu kwaajili ya kufadhili miradi mikubwa ya maendeleo yenye athari Chanya kwa jamii na uchumi.

Kupitia mradi wa upanuzi wa nishati ya umeme vijijini (Tanzania Rural Electrification Expansion Programme-TREEP), Benki inaendelea kushirikiana na Benki ya Dunia kupitia.

Kamati yapokea taarifa za ujenzi Jengo la Wizara ya Madini
Mafunzo ya Urubani: NIT yakamilisha taratibu kupata Ithibati ya TCAA