Zaidi ya Wananchi 4 000 wa Kata ya Hidet iliyopo Wilayani Hanang Mkoani Manyara, wameanza kunufaika na mradi wa maji kutoka Ziwa Bassoutghang baada ya kujengwa kwa mitambo ya kusafisha maji hayo na kuanza kutumika kwa matumizi ya binadamu.

Wakizungumza mara baada ya kuwekwa kwa jiwe la msingi katika mradi wa Ziwa Bassotughang, Wananchi hao wameelezea kero walizopitia kabla ya kujengwa kwa mradi huo uliowanufaisha.

Awali, Mbunge wa Jimbo la Hanang, Samuel Hayuma aliipongeza Serikali kwa kuwakumbuka Wananchi wa Kijiji hicho waliowekewa miundombinu bora ya upatikanaji wa maji.

Naye Meneja wa RUWASA Wilaya ya Hanang, Herbert Kijazi amesema mradi huo umegharimu zaidi ya Tshs. Bilioni 1.5 ambazo ni fedha za Serikali.

Uhujumu miundombinu ya SGR una athari - Kadogosa
Baraza la saba la Wafanyakazi Wizara ya Nishati lakutana Dodoma