Belinda Joseph, Songea – Ruvuma.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Manispaa ya Songea,  James Mgego amewakumbusha Wenyeviti na Wajumbe wa Serikali za Mitaa kutenda haki bila kubagua wananchi kwa itikadi zao za kidini na kitamaduni badala yake wafanye kazi kwa kutanguliza masilahi ya wananchi nasio yao binafsi kwani cheo ni dhamana.

Akizungumza wakati wakuhitimisha ziara ya Sekretarieti ya CCM Wilaya Songea Mjini katika kata 21 za Manispaa hiyo kwenye shule ya Dkt. Emmanuel Nchimbi Kata ya Msamala, Mgego amewataka wenyeviti na wajumbe waliopata ridhaa ya wananchi katika uchaguzi wa mwaka 2024, waende wakatende haki ili kuleta usawa katika jamii.

Amesema, katika kipindi chote cha ziara hiyo walijikita kutoa shukrani zao za dhati kwa wanachama na viongozi wa Jumuiya zote na wananchi kwa ujumla, kuendelea kukiamini chama kwa kukipatia ushindi wa asilimia 100 mwaka jana, huku matarajio yao ushirikiano huo huo uendelee hata katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025.

Mgego ameeleza kuwa, kila mwanachama wa CCM mwenye mapenzi na chama, anaruhusiwa kugombea nafasi za ubunge na udiwani kasoro nafasi ya urais ambayo nikwa Rais Samia, ambapo amewataka wanachama wakae wajipime wakiona wanatosha basi chama kitawapa nafasi ya kila mtu kugombea nafasi hizo wakati utakapofika.

Aidha, amebainisha kuwa katika kila kata asilimia kubwa ilani ya CCM imetekelezwa katika miradi mbalimbali ikiwemo barabara, ujenzi wa shule na vyumba vya madarasa vya kisasa, miradi mikubwa ya maji, pembejeo zakilimo kwa bei nafuu n.k, hivyo wananchi wamesema wanadeni kubwa kwa serikali na zawadi pekee kwa serikali ya awamu ya sita ni kura nyingi za kishindo kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Alihitimisha kwa kuwataka wanachama wa chama hicho kuutumia mwezi huu wa mfungo wa Ramadhani na Kwarezima, kuendelea kuiombea nchi amani, kukiombea chama cha mapinduzi pamoja na viongozi wa chama hicho kwaajili ya maendeleo.

New zealand yatinga Kombe la Dunia 2026
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 24, 2025