Mshambuliaji wa Newcastle Alexander Isak yuko tayari kuhamia Barcelona lakini angependelea kujiunga na Liverpool ikiwa watamnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden mwenye umri wa miaka 25 msimu huu. (El Nacional – in Spanish)
Kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin De Bruyne, 33, amefanya mazungumzo na klabu ya MLS San Diego kuhusu uhamisho wa bila malipo mkataba wake Manchester City utakapokamilika msimu huu wa kiangazi. (Sun)
Mshambuliji wa Bayern Munich Harry Kane, 31, anafikiria kurejea Uingereza msimu huu wa kiangazi, huku Liverpool ikiwa ni mahali anapopendelea zaidi. (Fichajes – in Spanish)
Chelsea lazima walipe Manchester United pauni milioni 5 ikiwa watachagua kupinga kugeuza mkopo wa mshambuliaji wa Uingereza Jadon Sancho kuwa mkataba wa kudumu. (Subscriotion is required)
Tottenham wameanza kuchunguza mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Southampton mwenye umri wa chini ya miaka 21 wa Southampton, Tyler Dibling. (Givemesport)
Liverpool wanatumai kumtumia winga wa Scotland mwenye umri wa miaka 19 Ben Doak katika mkataba wowote kama njia ya kumpata beki wa Bournemouth Milos Kerkez wa Hungary mwenye umri wa miaka 21 au fowadi wa Ghana Antoine Semenyo, 25. (Sun)
Liverpool wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez mwenye umri wa miaka 25 msimu huu wa kiangazi. (Football Insider)
Tottenham wanatazamia kuanza mazungumzo na kiungo wa kati wa Uruguay Rodrigo Bentancur, 27, kuhusu kuongezwa kwa mkataba wake, ambao unaisha msimu ujao wa kiangazi, huku kukiwa na nia ya AC Milan . (TBR Football)