Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Peter Msigwa amewataka Watanzania kupuuza habari za uongo dhidi yake zinazosambazwa na wabaya wake kisiasa, akisema taarifa hizo ni uzushi na hazina ukweli.
Kupitia andiko lake la mtandao wa kijamii, Msigwa ameanduka kuwa, “Puuzeni uongo huu, hauna ukweli wowote umetungwa na watu waliojipa majukumu ya kunisemea wakati wanajua uwezo wa kujisemea mwenyewe ninao.”

Taarifa hizo, zinaeleza kwamba Msigwa amepanga kurejea katika chama chake cha zamani Chadema, Machi 29, 2025 mjini Iringa, jambo ambalo hata hivyo amelikanusha.