Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limesajili jumla ya miradi 8,058, ambapo kati yahiyo, 5,784 ni ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) na 2,274 ni ya Ukaguzi wa Mazingira.

Akizungumza na Waandishi wa habari Leo Machi 24, 2025 Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Immaculate Semesi amesema Vikao 3,836 vya wataalam vilifanyika kwa ajili ya kufanyamapitio  ya taarifa za TAM na Ukaguzi wa Miradi  nakutoa mapendekezo  ya maboresho  ya masuala yamsingi  ya kuzingatiwa  katika   taarifa hizo.

“Miradi4,570 iliidhinishwa na kupewa vyeti vya mazingira, Kati ya hivyo, 3,058 ni vya TAM, 765 ni vya Ukaguzi, hukuvyeti vingine vikiwemo vya kubadili masharti 169, vyeti vilivyohamishwa umiliki 552, vyeti vya muda (PEC) 53 na cheti kilichorudishwa Katika kuboresha utoaji wa huduma za vibali vya TAM, Baraza lilianzisha mfumo wa kielectroniki unaotumika hadi kuidhinishwa  kwa miradi ya TAM  ambao umeongezwa ufanisi,” amesema.

“Kabla ya mfumo Baraza lilikuwa linasajili takribani miradi 900 kwa mwaka na baadaya mfumo  Baraza linasajili  zaidi ya miradi 2,000  kwa mwaka, haya ni mageuzi makubwa ya Serikali ya   awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia SuluhuHassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Semesi.

Hata hivyo amesema Katika kipindi cha mwaka 2020/21- 2024/25, Baraza limefanikiwa kusajili wataalam Elekezi wa Mazingira 1,023  na kutoa vyeti vya utendaji kwa Wataalam Elekezi503 baada ya kukidhi vigezo  kwa mujibu wa Kanuni  za Usajili  na utendaji wa Wataalam Elekezi wa Mazingira za mwaka 2021.

“Kanuni hizi mpya zimeongeza ufanisi kwa kuruhusu  usajili  kufanyika wakati wowote. Usajiliwa Wataalam Elekezi wa Mazingira unafanyika kupitia mfumo wa kielektroniki ambao umeongeza  ufanisi wakushughulikia maombi,” amesema.

“Katika suala zima la elimu kwa umma linalosisitiza uhamasishaji na kuzuia Madhara yamatumizi ya mifuko ya Plastiki, Baraza limefanikiwakuandaa vipindi 88 vya uhamasishaji kupitia vyombovya habari na mikutano 20 ya wadau kuhusu madhara yamatumizi ya mifuko ya plastiki”. Amesema Semesi

Vilevile amesema kaguzizilifanyika katika maeneo 178 ya uzalishaji nausambazaji wa mifuko ya plastiki, ambapo maeneo 57 yalikutwa na makosa na kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria.

“Zaidi ya Tani 150 za vifungashio visivyokidhiviwango vilikamatwa, vikataifishwa na kuteketezwa kwa mujibu wa Sheria”, amesema

“Hata hivyo suala la udhibi wavifungashio vya plastiki ni letu sote  kuanzia ngazi yafamilia hadi Taifa  hivyo hatuna budi kushirikiana kwa ajili ya  kuleta matokeo chanya”. Amesema Semesi.

 

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 25, 2025
Msigwa ataka jamii ipuuze taarifa za uvumi juu yake