Wakala wa Vipimo (WMA) inatarajia kuanza uhakiki wa Taxi meter ambapo umenunua mitambo 12, miwili ya imesimikwa mmoja unaendelea kusimikwa katika kituo cha uhakiki wa Vipimo Misugusugu Mkoa wa Pwani na mwingine utasimikwa katika ofisi ya Makao Makuu Dodoma.

Akizungumza na Waandishi wa habari Leo Jijini Didoma Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Alban Kihulla amesema mitambo mingine 10 (portable taximeter) itagawiwa kwenye mikoa kwa ajili ya kuhakiki vipimo mwendo kwenye vyombo vya usafiri.

Hata hivyo amesema Katika Kutekeleza Mpango wa Matumizi ya Gesi Asilia kwa kujenga miundombinu na kuhamasisha matumizi ya gesi asilia viwandani, majumbani, kwenye taasisi mbalimbali na kwenye vyombo vya usafiri ili kupunguza uharibifu wa mazingira, Wakala wa vipimo inafanya uhakiki wa mita zote zinazotumika kupima gesi asilia (CNG).

“Zinaanzia inapochakatwa hadi inapofika kwa watumiaji wa mwisho kwenye vituo maalumu vya kuuzia gesi vilivyopo Tazara, Ubungo, Dangote (Mkuranga & Mtwara), Taqwa Airport na Mlimani City, TPDC (Mlimani City) na Mandela Road (Tembo Energies),” amesema.

“Pia, WMA inahakiki uzito wa mitungi ya gesi ambayo inafungwa kwenye vyombo vya usafiri ili kujiridhisha usahihi wa vipimo wake,” amesema Kihulla.

Hata hivyo amesema wanaendelea kufanya kaguzi katika bidhaa zilizofungashwa na kwamba bidhaa iliyofungashwa ni yoyote inayouzwa kwa vipimo vya uzito, ujazo, urefu, namba au unene na iliyofungashwa ppasipona uwepo wa mnunuaji.

“Mfano wa bidhaa zinazofungashwa kwa uzito ni kama vile saruji, unga na sukari.Zinazofungashwa kwa ujazo (asali, soda na maji), urefu (nondo, mabati, waya, n.k), namba (njiti za kiberiti, sigara), unene (nondo, mabati),” amesema Kihulla

Amesema Kwa muktadha huo, bidhaa zote zinazozalishwa ndani ya nchi na zile zinazoingizwa kutoka nje ya nchi zinahakikiwa na Wakala wa Vipimo.

Ameongezea kwa kusema Wakala umejipanga kuendelea kufungua ofisi sehemu mbalimbali zinazooneka kuwa na ukuaji wa shughuli za ukuaji wa kiuchumi na kijamii ili kuendelea kuwalinda watoa huduma na wapokea huduma kupitia matumizi ya vipimo vilivyohakikiwa.

Mradi wa Maji, Barabara kuwanufaisha zaidi ya 5,000 Kilindi - Mbinga