Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limefanikiwa kuunganisha Gridi za umeme za Taifa kati ya nchi ya Kenya na Tanzania kufuatia kukamilika Kwa Mradi wa Kituo cha Kupoza na Kusafirisha Umeme cha Lemuguru kilichopo Arusha.

Akizungumza na Waandishi wa habari Leo Machi 26, 2025, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi, Gissima Nyamo amesema Muunganiko huo umekamilika na Gridi kuunganika kwa kupitia laini ya usafirishaji Umeme kutoka Arusha kwenda Kenya, ambayo iliwashwa tarehe 13 Disemba, 2024.

“Hatua hii inaifanya Tanzania kuwa katika muunganiko wa kikanda wa nchi za Afrika Mashariki katika Umeme yaani (Eastern Africa Power Pool)”, amesema

Pia amesema wameendelea na Utekelezaji wa Mradi wa Usafirishaji wa Umeme kutoka Tanzania hadi Zambia (TAZA).

“Ambapo Tanzania itaungana na mtandao wa Gridi wa Jumuiya ya Nishati katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika yaani Southern Africa Power Pool (SAPP)”, amesema

“Mradi huu wa njia ya kusafirisha umeme  wa msongo wa kV 400 kutoka Iringa kupitia Mbeya, Tunduma hadi Sumbawanga (TAZA) yenye urefu wa kilomita 624 pamoja na vituo vyake vya kupoza umeme katika maeneo hayo, Utekelezaji wa mradi unaendelea na hadi kufikia sasa umefikia asilimia 34 na unategemewa kukamilika Mei 2026”. Amesema Mhandisi Nyamo

Vile vile amesema Serikali kupitia TANESCO ilifanikiwa kuanzisha Miradi ya kuimarisha miundombinu ya mfumo wa Gridi ya Taifa uitwao Gridi Imara ambao lengo lake ni kuimarisha miundombinu ya njia za kusafirisha umeme.

“Na kusambaza umeme, kupanua vituo vya kupoza umeme, kujenga njia mpya za kusafirisha umeme, Ujenzi wa vituo vya kupoza umeme, ubadilishaji wa nguzo za miti kusimika za zege na ufungaji wa transfoma ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme wa uhakika katika mfumo wa Gridi ya Taifa utekelezaji wake umefikia asilimia 40ambapo miradi sita (6) kati ya 27 imekamilika na unategemewa kukamilika mwaka wa fedha 2026/2027”, amesema

Geita: Wakamatwa wakisafirisha Dhahabu kwa magendo
Chatu wazua taharuki Katavi, Wananchi waomba msaada