Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda miundombinu ya mawasiliano ili kuhakikisha huduma za mawasiliano zinadumu na kuwa bora zaidi.

Naibu Waziri Mahundi alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya mawasiliano katika Jimbo la Tabora Kaskazini katika Kata ya Ifucha na kuongeza kuwa miradi ya mawasiliano inajengwa kwa gharama kubwa, hivyo ni jukumu la kila mwananchi kushiriki katika kuitunza na kuilinda miundombinu hiyo dhidi ya uharibifu au wizi.

Amezitaka kampuni za simu kuhakikisha wanalipa walinzi wa minara ya mawasiliano kwa wakati ili kuongeza ari ya wafanyakazi hao kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

“Rais Dkt. Samia anapenda amani, na anapoleta miradi ya maendeleo kama hii, anapenda muitumie kwa amani,” alisisitiza Naibu Waziri Mahundi.

Awali, akitoa taarifa kuhusu mnara huo, Kaimu Meneja wa Muko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Shirikisho Mpunji alisema kuwa mara huo ni miongoni mwa minara 758 ya mawasiliano inayojengwa kwa ruzuku ya Serikali kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali ambapo Serikali imechangia shilingi milioni 109 kwa ajili ya ujenzi wa mnara huo unahudumia wakazi wa kijiji cha Kazima.

Tutafanyia kazi Taarifa ya TAKUKURU, CAG - Rais Samia
Ukiukwaji wa Maadili: Sita wafikishwa mbele ya Baraza