Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ipo tayari kufanyia kazi maoni na mapendekezo yaliyotolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na ile iliyotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG, Charles Kichere.

Rais Samia ameyasema hayo katika hafla ya kupokea taarifa ya Mwaka ya CAG na TAKUKURU iliyofanyika hii leo Machi 27, 2025 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amesema, “sisi upade wa Serikali tuko tayari kuendelea kufanyia kazi maoni na mapendekezo yaliyotolewa ndani ya taarifa hizi mbili, tutasikiliza vizuri, tutafuatilia vizuri mjadala wa bunge kwenye taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali.”

“Lakini pia kwa taarifa ya TAKUKURU. Tutakwenda kufanyia kazi vizuri yale yote ambayo yameelezwa ili hatimaye tuweze kujenga utawala bora ndani ya nchi yetu,” amesema Rais Samia.

Deni la Serikali limefikia Trilioni 97.35 - CAG Kichere
Wananchi wasisitizwa kulinda miundombinu ya mawasiliano