Hadi kufikia Juni 30, 2024 Deni la Serikali lilifikia shilingi trilioni 97.35 likiongezeka kutoka shilingi trilioni 82.25 kwa mwaka wa Fedha 2022/2023, ambalo ni ongezeko la shilingi Trilioni 15.1 sawa na asilimia 18.36.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere ameyasema hayo kwenye hafla ya kupokea taarifa ya Mwaka ya TAKUKURU na ripoti ya CAG kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Ikulu jijini Dar es salam, hii leo Machi 27, 2025.

Amesema, deni hilo linajumuisha deni la ndani la Shilingi Trilioni 31.95 na deni la nje la shilingi Trilioni 65.40 huku akidai tathimini imebaini kuwa deni hilo la Taifa, bado ni himilivu.

Kuna upungufu wa vyakula vyenye protini Vijijini - Nchimbi
Tutafanyia kazi Taarifa ya TAKUKURU, CAG - Rais Samia