Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imeielekeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kuhakikisha inazingatia miongozo na kanuni katika utekelezaji wa miradi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Halima Mdee ametoa maelekezo hayo baada ya ukaguzi wa miradi miwili ambayo ni nyumba ya Mkurugenzi wa Halmashauri na kukagua mradi wa wodi tatu (wanaume, wanawake, na watoto) katika hospitali ya Halmashauri.

“Ofisa Masuhuri ahakikishe miradi yote inayotekelezwa inafuata miongozo, sheria, na kanuni zinazotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI,” amesisitiza.

Amesema kamati imeongeza kuwa matumizi sahihi ya miongozo, sheria, na kanuni ni muhimu katika kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia thamani ya fedha na kuepusha matumizi mabaya ya rasilimali.

Maisha: Nilivyokutana na muujiza wa kupona kifua kikuu
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 27, 2025