Mtoto Ibrahim Masumbuko (9), Mwanafunzi wa Darasa la kwanza Shule ya Msingi Kakoyoyo Mkoani Geita, amepoteza Maisha kwa kupigwa na radi, ambayo pia iliwajeruhi Watoto wawili Kulwa Masumbuko (11), Mwanafunzi wa Darasa la Tatu katika Shule hiyo na Isaka Masumbuko (3), wote wa familia ya Masumbuko Lushona.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Adam Maro amesema tukio hilo lililotokea Machi 23, 2025 majira ya saa 12 jioni, katika Kitongoji cha Igwamanoni, kilichopo Kijiji cha Kakoyoyo Wilayani Bukombe, Mkoani Geita.

Amesema, siku ya tukio ilinyesha mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na radi ambapo watoto hao walikuwa kwenye mashamba ya mpunga wakiwinda ndege, baada ya kuona mvua kubwa walianza kukimbia kurudi nyumbani na wakiwa njiani, walipigwa na radi na kusababisha kifo na majeruhi kwa watoto hao.

TRC imepata hasara ya Bil. 224, TTCL ni Bil. 27.78 - CAG
Wauguzi Viongozi watakiwa kusimamia utoaji huduma bora za Afya