Taasisi Ya Jiolojia na utafiti wa
Madini Tanzani (GST) imeendelea kuongeza makusanyo ya ndani kutoka wastani wa shilingi 1,251,428,472.91 mwaka 2021 hadi shilingi 2,394,211,348 mwaka 2023/2024, sawa na ongezeko la asilimia 91.32.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Nokta Banteze ambapo amesema Ongezeko hilo limepatikana kupitia mageuzi na maboresho mbalimbali ya kiutendaji yaliyofanyika katika kipindi husika ambayo yaliongeza ubora wa huduma zitolewazo na GST.
“ vilevile Kuongezeka kwa idadi ya sampuli zinazochunguzwa kutoka wastani wa sampuli 19,184 mwaka 2021 hadi sampuli 25,793 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 34.45,” amesema.
“Ongezeko hili limetokana na maboresho makubwa ya maabara yaliyofanyika hasa katika ununuziwa vifaa na mashine za kisasa za uchunguzi wa sampuli”. Amesema Banteze
Hata hivyo amesema GST ilikamilisha ugani wa jiolojia kwa lengo la kubaini miamba na madini yanayopatikana kwenye QDS278 na 290 zilizopo Hifadhi ya Taifa ya Mwalimu Nyerere na Pori la Akiba la Selous – katika sehemu ya Mikoa wa Lindi na Ruvuma).
“Lakini pia QDS mbili (2) mpya ambazo ni QDS 203 na 204 katika sehemu ya Mkoa wa Pwani na sehemu ndogo ya Mkoa wa Dar es salaam, na Matokeo ya awali ya utafiti yanaonesha uwepo wa mchanga wa ujenzi, madini ya dhahabu na uranikwenye QDS 278 na 290,” amesema.
“ Na uwepo wa madini ya kaolin, chokaa, udongo mfinyanzi, silica sand, madini tembo (heavy mineral sands) na metali adimu (rareearth elements) kwenye QDS 203 na 204, (note, QDS ni quarter degree sheet eneo lenye ukubwa wa kilometer 54 kwa 54.” amesema Banteze.
Vilevile amesema GST kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilikamilisha utafiti na uchoraji wa ramani ya jiolojia ya visiwa vya Zanzibar (Unguja na Pemba).
“Ikumbukwe kuwa visiwa vya Zanzibar havijawai kufanyiwa utafiti huo wa jiolojia, Matokeo ya utafiti huo yamebaini uwepo wa miamba ya chokaa yenye ubora wa kutengeneza saruji, madini tembo (heavy mineral sands), madini ya silica, strontium, vyanzo vya maji ardhi, maeneo yenye vivutio vya utalii wa jiolojia na maeneo hatarishi kwa majanga ya asili ya jiolojia,” amesema.