Afarah Suleiman, Babati – Manyara.
Baada ya kusambaa kwa Taarifa ya kuchomwa moto Nyumba ya Mwananchi wa Mtaa wa Maisaka kati Mbunge wa jimbo la Babati Mjini, Pauline Gekul amejitokeza kuifariji Familia ya mwananchi huyo, nakuwasihi Wadau wenye mapenzi mema kuendelea kumsaidia muhanga wa tukio hilo.
Akizungumza na mwananchi huyo Gekul amesema amesikitishwa na tukio hilo, nakutoa mkono wa pole huku akiahidi kusimamia michango mbalimbali ya wadau inayochangishwa kwa lengo la kumjengea nyumba ya mwananchi huyo.
Aidha, Gekul amesema baada ya kuona Taarifa ya tukio hilo, ameamuwa kuwashirikisha wadau Mbalimbali katika makundi sogozi ili kumfariji mwananchi huyo huku akiliomba jeshi la polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo na kuabaini waliohusika.
Mwenyekiti wa Baraza la wazee Wilaya ya Babati, Juma Mkola ameshangazwa na tukio hilo na kuwasihi wananchi kuwa msari wa mbele katika kukemea matukio ya namna hiyo ili lisijirudie kwa mwananchi mwingine.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Maisaka na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Abrahaman Kololi amelaani tukio hilo na kuahidi kushirikiana na mbunge katika kufanikisha ujenzi wa nyumba ya mwananchi huyo.
Naye, Husna Hassa Hussein Mwananchi aliyechomewa Nyumba amemshukuru mbunge Gekul kwa namna alivyoguswa na tukio hilo pamoja na wadau wengine wengine kwa kumsaidia.