Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Jumuiya ya Vijana wa Kiislam BAKWATA Mkoa wa Manyara, imefanya mashindano ya tatu ya kuifadhi Quran tukufu yaliyoshirikisha mikoa mitatu ikiwemo Arusha na Dodoma.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emanuela Kaganda amewataka viongozi wa dini wakiwemo Mashekhe kusimamia vyema maadili ya watoto kwa kuendelea kuwafundisha yaliyo agizwa na mwenye enzi MUNGU, huku akiahadi kushirikiana nao.

Aidha kaganda ametoa wito kwa viongozi hao wa dini pamoja na wananchi kwa ujumla kuendelea kuliombea Taifa katika kipindi hichi ambacho nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu 2025..

Kwa upande wake Mbunge wa Vijana Taifa, Asia Halamga ambaye pia ni mlezi wa mashindano hayo ya kuhifadhi Quran mkoa Manyara kwa miaka mitatu amesema mashindao hayo yanasaidi vijana kumjua mwenyezi mungu na mafundisho yake.

Naye mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana wa kiislamu Bakwata mkoa wa Manyara (JUVIKIBA) Abdulkarim yusufu shaban amesema wanatarajia mashindao hayo kuwa zaidi ya mikoa mitatu hivyo ,amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kudhamini mashino hayo.

Katibu wa Jumuiya ya vijana wa kiislmu mkoani humo Shafii Mmbwana ametoa shukrani kwa serikali ya wilaya na mkoa pamoja na wazazi kwa kuunga mkono mashindano hayo.

CCM yawonya watakaochafua hali ya hewa baada ya Ramadhan
TANESCO yashinda tena Tuzo CICM ubora wa huduma kwa Wateja