Belinda Joseph, Madaba – Ruvuma.

Mbunge wa Jimbo la Madaba, Dkt. Joseph Kizito Mhagama, ameeleza mafanikio ya utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa kipindi cha miaka mitano yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 7.69 katika Kijiji cha Lituta, Kata ya Lituta, Akizungumzia maendeleo katika sekta ya elimu, barabara, maji, na afya, Mhagama alisema kuwa hospitali ya wilaya imemalizika na sasa inatoa huduma bora kwa wananchi, ikiwa na vifaa vyote muhimu.

Katika mkutano wake na wananchi wa kijiji hicho, Mhagama amesisitiza kuwa serikali inaendelea kuwekeza katika maeneo hayo ili kuboresha maisha ya wakazi wa Madaba, Ameelezea kuwa ujenzi wa barabara na madaraja unaendelea na zaidi ya shilingi bilioni 1.5 zimetumika katika mradi huo, ameahidi kuwa barabara zote za lami katika Halmashauri ya Madaba zitajengwa na mradi wa maji utaimarishwa ili wananchi wapate huduma bora za maji safi na salama

.

Mbunge huyo pia amechukizwa na vitendo vya wizi vilivyofanywa na baadhi ya watu walioiba vifaa vya Hospitali ya Halmashauri ya Madaba, akisema wahusika wamebainika na hatua za kisheria zimechukuliwa dhidi yao. Alisisitiza umuhimu wa kulinda miundombinu ya umma na kuwataka wananchi wa Lituta na Madaba kwa ujumla kudumisha mshikamano ili kuendelea na maendeleo yaliyopatikana.

Mhagama amefafanua kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya juhudi za pamoja na akiwasihi wananchi kushirikiana na kuepuka vitendo vya uharibifu ambavyo vinaweza kuvuruga maendeleo yao, ametumia fursa hiyo kutoa shukrani kwa wananchi wa Lituta kwa msaada wao mkubwa katika kumsaidia kuchukua tena fomu ya ubunge kwa uchaguzi wa mwaka huu, ambao waliamua kuchanga fedha hizo na kumuomba angombee tena nafasi hiyo kwani bado wanamuhitaji kwa mustakabali wa maendeleo ya Jimbo hilo.

Mbunge huyo amewataka wananchi wa Lituta na Madaba kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao, kwa kuchagua viongozi wanaoleta maendeleo kwa Jimbo la Madaba, akisisitiza kuwa maendeleo ya eneo hilo ni lazima yaendelee kwa manufaa ya wote.

Akizungumza kwaniaba wazee wa kijiji cha Lituta, amempongeza Mbunge huyo akieleza mabadiliko yaliyopo kwasasa katika Jimbo hilo akieleza namna ambavyo wanatamani kurudi ujana ili waweze kufurahia zaidi mafanikio yaliyopo hususani kwenye wodi za wanawake hospitali wanapokwenda kujifungua, kufuatia huduma za afya kuboreshwa hivyo wao kama wazee waeneo hilo hawana chakumlipa Mbunge zaidi ya kura nyingi mwaka huu.

Kwa upande wa mwakilishi wa Vijana Posko Mgunda, ameeleza kuwa kwasasa wao kama wazaliwa wa eneo hilo wanaifahamu Madaba ilivyokuwa awali na ilivyosasa hivyo hawakitayari kusikiliza maneno ya watu watakaopotosha kuhusiana na Jimbo hilo badala yake wataungana nakuunga mkono uchapakazi wa Mbunge Joseph Kizito Mhagama.

Maisha: Laana, roho mbaya zilivyonitesa katika mapenzi
Gekul amshika mkono mwananchi aliyechomewa nyumba