Chama cha Mapinduzi – CCM, Mkoa wa Tanga, kimewaonya watu wote wataotaka kufanya vitendo visivyo vya kiungwana ikiwemo ikiwemo wanasiasa kupandikiza chuki miongoni mwa Jamii.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Abdarhaman Rajab aliwaambia Waandishi wa Habari leo,wakati akitoa Salamu za Eid kwaniaba ya chama hicho mbele ya Waandishi wa Habari jijini Tanga,

“Wale wote waliojipanga kwa ajili ya kufanya siasa zenye viashiria vya kuvunja amani,hatutamuonea haya, waje kwa adabu watakapoingia kule mpakani mwa Mkoa wetu wa Tanga vinginevyo hatutawavumilia, Tanga kipaumbele chetu ni kulinda amani,” aliongeza Rajab.

Aliwataka waumini wa Dini ya Kiislamu kuendeleza yale yote Mazuri waliyoyatekereza wakati wa mfungo wa Ramadhan,

” Niwaombe Waislamu wenzangu,tuendeleze mema yote tuliyoyatekereza wakati wa mfungo wa Ramadhan, tusije tukaanza kufanya maasi kwakisingizio kuwa Ramadhan imekwisha ” Aliongeza Rajab

Aidha kuhusu Amani na utulivu, Mwenyekiti huyo alisema, Mkoa wa Tanga umejipanga kuhakikisha Wananchi wanasherekea kwa Amani na utulivu,

“Chini ya Mwenyekiti wetu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama,Dkt.Batilda Buriani,tumejipanga kuhakikisha Wananchi wetu wanasherekea kwa Amani, tunaamini kila mmoja wetu atakuwa mlinzi wa mwenzake,CCM Mkoa wa Tanga inawatakia kila la kheri ya Eid El Fitr,” alisisitiza.

Maisha: Fanya hivi kupata faida kubwa katika biashara
DC Kaganda ataka usimamizi maadili ya Watoto, Vijana