Rais wa Kenya, William Ruto amemshtumu aliyekuwa Naibu wake Rigathi Gachagua ambaye aliondolewa madarakani kuwa aliwahangaisha Wabunge na Wafanyakazi wa Ikulu, alipokuwa madarakani.
Ruto ambaye yupo katika ziara ya siku tano huko Mlima Kenya, eneo ambalo ni ngome ya kisiasa ya Gachagua ameyasema hayo wakati wa mahojiano na vyombo vya Habari.
Amesema, mara baada ya kuondolewa madarakani, Gachagua amekuwa mpinzani wake mkubwa wakati ambao wanaelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027, huku akisema Kiongozi huyo si mkweli.