Afarah Suleiman, Simanjiro – Manyara.

Mkoa wa Manyara leo Aprili 4, 2025 umefanya tukio maalumu la kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika Kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro, maadhimisho hayo kwa upekee yamepewa jina la *”SHUKA DAY; Minne ya Mafanikio, Maendeleo kwa wote”

Akiongoza maadhimisho hayo Mkuu wa mkoa wa Manyara, Queen Cuthbert Sendiga ameeleza miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Maji, Kilimo, Madini, Mifugo, Utalii nakadhalika.

Sendiga ameueleza wananchi wa kata hiyo kwamba kwa kipindi hichi cha miaka minne Mkoa wa Manyara umepokea zaidi ya Bilioni 700 kwajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ma ndeleo.

Aidha Sendiga, ameeleza umuhimu wa maadhimisho hayo kwani inatoa fursa ya kufanya tathimini ya hatua zilizopigwa na mafanikio yaliyopatikana kwenye maeneo ya mkoa kuanzia kitongoji, kijiji, Tarafa, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumala.

Mwisho kwa niaba ya wananchi Sendiga, amemshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwakuendelea kuwajali wananchi wa mkoa wa Manyara kwa kuridhia na kutoa fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani Manyara.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 5, 2025
Nguvu ya Kalamu ilete amani, mshikamano si vurugu – Dkt. Nchimbi