Swaum Katambo – Nsimbo.
Mbunge wa Jimbo la Nsimbo, Anna Lupembe ameendelea na ziara yake katika halmashauri ya Nsimbo ambapo ameweka mawe ya msingi katika miradi ya elimu yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 228.
Akiwa katika Kijiji cha Usense ameweka jiwe la msingi vyumba vinne vya madarasa na matundu 6 ya vyoo vya Shule ya Msingi Usense na kuelekekea Shule ya Sekondari Anna Lupembe kuweka jiwe la msingi ujenzi wa nyumba ya Mwalimu.
Lupembe amesema hatua hizo ni katika kuboresha miundombinu ya elimu na kuweka mazingira sawa ya ujifunzaji kwa wanafunzi na ufundishaji kwa walimu kwa kuwaweka karibu na mazingira ya shule ili kuboresha mazingira bora ya elimu.
Baada ya kuweka mawe ya msingi Lupembe amefanya mkutano wa hadhara na kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwa wananchi katika vijiji vya Usense na Isanjandugu na kero hizo kupatiwa majibu.