Uongozi wa Kiwanda cha kuzallisha vioo cha KEDA kilichoko Mkuranga Mkoa wa Pwani, unatarajia kuongeza nafasi za ajira kwa Vijana kutoka 506 za sasa hadi 1000.

Hatua hiyo, inatajwa kuleta matumaini na faraja kwa kundi la Vijana ambao asilimia kubwa wamekuwa wakihangaika kutafuta ajira.

Meneja wa kiwanda hicho, Nuhu Changawa akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya mwenge wa uhuru kutembelea maendeleo ya upanuzi wa majengo unaoendelea amesema kipaumbele cha nafasi za ajira kitakuwa kwa vijana wazawa.

Kwa upande wake Afisa biashara wa kiwanda hicho, Masoud Suleywan amesema kuwa ili kulinda hadhi na heshima ya kampini yao wameendelea kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa.

Kwa upande wake Afisa biashara wa kiwanda hicho, Masoud Suleywan amesema kuwa ili kulinda hadhi na heshima ya kampini yao wameendelea kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa.

 

Kiongozi Mkuu wa Kiwanda hicho, Tony Wu amesema kilichowavutia kuja kuwekeza nchini Tanzania ni kutokana na sera na sheria nzuri zilizopo.

Awali, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa 2025, Ismail All Ussi amewataka vijana wanaopata ajira kwenye viwanda kufanya kazi kwa uaminifu ili kulinda heshima ya nchi.

Amesema, Serikali inaendelea kuwaita wawekezaji kwa kutambua kuwa wanachangia kueleta mandeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

TRA yavuka lengo ukusanyaji wa Mapato miezi tisa mfululizo
Teuzi: Sirro Mwenyekiti mpya wa Bodi STAMICO