Afarah Suleiman, Mbulu – Manyara.
Serikali Nchini, imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika kipindi cha awamu ya sita ya Rais dkt.Samia suluhu hasssan, ambapo Wilaya ya Mbulu imepokea zaidi ya shilingi bilioni 200 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Michael john Semindu, amesema kuwa fedha hizo zimeelekezwa katika miradi ya sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, maji, barabara na kilimo na kuwataka wananchi wilayani humo kuitumia vyema na kuilinda miradi hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbulu, Comrade Melkiadi jacobo amesema kuwa miradi mingi iliyotekelezwa chini ya uongozi wa Rais Samia suluhu hassan katika kioindi chake cha miaka minne imewagusa zaidi wananchi moja kwa moja na kuleta tija katika maendeleo yao ya kila siku.aidha
Aidha Wananchi wa wilaya ya Mbulu wameishukuru serikali ya awamu ya sita inqyoongozwa na dkt.samia kwa kutekeleza miradi hiyo ya maendeleo na kuwanufaisha.