Ni shangwe na furaha kwa waumini wa Kanisa la AICT Mpanda ikiwa ni kuonesha shukrani za dhati mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuchangia ujenzi wa kanisa hilo kwa kutoa kiasi sh milioni 50 ambazo zimeshaingizwa kwenye akaunti ya kanisa.
Akitoa salamu za upendo kwa niaba ya Rais Samia,Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema Serikali ya mkoa ilimshirikisha Rais katika suala la ujenzi wa kanisa hilo ambapo ameweza kuchangia ujenzi wa kanisa.
Mrindoko amezungumzia suala la maadili kwa kuwataka wananchi kuwaongoza na kuwajenga watoto na vijana katika maadili mema kwa kukemea vitendo vyote viovu ambavyo ni kinyume na maadli ya kitanzania huku akisisitiza suala la amani,upendo na mshikamano ndani ya jamii.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Kanisa, Mwinjilisti Joel Nkanda amesema wamepokea kwa moyo wa shukrani fedha hizo na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kuendeleza amani na mshikamano.