Waziri, Kassim Majaliwa amesema utekelezaji wa maboresho ya kisera na mipango mbalimbali katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo zinasimamiwa na TAMISEMI na Wakuu wa Mikoa umewezesha kuleta mafanikio yanayogusa moja kwa moja maisha ya kila siku ya wananchi kwenye sekta za huduma za kijamii.
Majaliwa ameyasema hayo wakati wa Mkutano Mkuu wa 15 wa TOA unaofanyika katika Ukumbi wa Jiji la Dodoma na kuongeza kuwa utekelezaji wa maboresho ya kisera na mipango mbalimbali katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo zinasimamiwa na TAMISEMI na Wakuu wa Mikoa umewezesha kuleta mafanikio yanayogusa moja kwa moja maisha ya kila siku ya wananchi kwenye sekta za huduma za kijamii.
Kuhusu mifumo ya kielektroniki, Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Sita imesimamia matumizi yake ili kuimarisha ufanisi, uwazi na uwajibikaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Amesema, “mifumo hiyo ni pamoja na Mifumo ya Uhasibu, Mifumo ya ukusanyaji wa mapato, Manunuzi na Malipo. Matumizi ya Mifumo yamesaidia kupunguza urasimu, kurahisisha ulipaji wa malipo na kodi mbalimbali za Serikali na kuboresha ukusanyaji wa mapato hadi kufikia ukusanyaji wa zaidi ya shilingi bilioni 900.”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuagiza uongozi wa TOA uwajibike kuhamasisha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutanua wigo wa mapato ili kuongeza uwezo wa kujitegemea kimapato na kugharamia shughuli mbalimbali za uendeshaji na utoaji wa huduma.