Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amewataka viongozi wote wa Mikoa na watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini, waendelee kusimamia maadili na uzalendo, mifumo ya ukusanyaji wa mapato pamoja na mifumo mingine yote iliyoanzishwa na Serikali kwenye ngazi zao.
Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa Mkutano Mkuu wa 15 wa TOA unaofanyika katika Ukumbi wa Jiji la Dodoma na kuwasisitiza viongozi hao waendelee kusimamia kikamilifu matumizi ya fedha za umma.
Aidha, amewataka kusimami pia utoaji wa huduma bora kwa wananchi, kwani kumekuwa na ufanisi zaidi katika Serikali za Mitaa.
Awali, Mwenyekiti wa Taifa wa Taasisi ya Maboresho ya Serikali za Mitaa Tanzania, Albert Msovela alisema wataendelea kusimamia taasisi hiyo na kuhakikisha wanatekeleza shughuli zote za Serikali kwa weledi na ufanisi mkubwa.