Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda kuhakikisha anamsimamia mkandarasi anayetekeleza mradi wa Shule mpya ya Sekondari Kanda ya Magharibi Katavi Boys, kufanya kazi usiku na mchana ili kufikia Mei 31 mradi huo kukamilika.

Mrindoko ametoa maagizo hayo mara baada ya kutoridhishwa na maelezo aliyoyapata kuhusu mradi huo pamoja na kasi ya utekelezaji wa mradi huo ambao mpaka sasa umefikia asilimia 65.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Mpanda, Paul Kahoya ameahidi kufanya kila jitihada kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.

Naye Mhandisi wa Ujenzi Mkoa wa Katavi, Sitta Masongo amesema changamoto iliyosababisha mradi huo kusuasua ni fundi kuwa na tenda zaidi ya moja jambo linalomfanya kutotekeleza mradi kama inavyotakiwa.

663 Wahitimu mafunzo ya kujenga Taifa Kibiti
Mchengerwa ahimiza uwajibikaji mifumo ukusanyaji wa mapato