Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema Daraja la Kigongo -Busisi limekamilika na mpaka kufikia Mwezi Mei 2025 litazinduliwa Rasmi.
Ametoa kauli hiyo Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na kusema miongoni mwa mambo makubwa yaliyofanywa Serikali ni pamoja na miradi ya kielelezo ya kimkakati kama Daraja la Kigongo-Busisi, Daraja la pangani, daraja la Tanzanite lililopo Dar es salaam na miradi mikubwa mingine inayoendelea.
Amesema, katika miaka minne ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan jumla ya kilomita za lami 1365 zimekamilika Nchini kote.