Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga ametoa siku 14 kwa waliovamia mashamba ya Wilaya ya Simanjiro kuondoka mara moja.

Sendiga ametoa agizo hilo akiwa katika Kijiji cha Landanai kilichopo Kata ya Nabelela Wilayani Simanjiro, kwenye mkutano wa hadhara, katika mwendelezo wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za Wananchi.

Awali  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Fakii Lulandala  alisema migogoro mingi katika kata hiyo, husababishwa na baadhi wanasiasa wasio kuwa waadilifu.

Kikwete afikisha ujumbe Maalum wa Rais Samia Congo Brazzaville
Ulega: Daraja la Kigongo - Busisi kuzinduliwa Mei 2025