Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Wizara imejipanga kuhakikisha inatatua changamoto ya maji kutokana na ongezeko la watu katika jiji la Dodoma ikiwa ni sehemu ya mkakati wa wizara hiyo.

Aweso ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma April 15, 2025 wakati wa halfa ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa majisafi Nzuguni awamu ya pili ambapo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imeingia mkataba na mkandarasi Bahaji Construction work wenye thamani ya shilingi Bilioni 5.6.

”Mradi huu utakwenda kwa miezi 15, mimi sio injinia wa maji lakini nimefanya kazi humu takribani mwaka wa nane unaenda wa tisa, mzee wangu Mkurugenzi wa Bahaji si mradi wa kufanya miezi 15 ni mradi wa kufanya miezi 6 au saba twendeni kwenye uelekeo huo wa kukamilisha mradi mapema watu wanufaike na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,” amesema Aweso

Amesema wizara hiyo haitakuwa kikwazo katika kuhakikisha wakazi wa Dodoma wanapata Majisafi na salama.

Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph amesema mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi 15 ambapo zaidi ya wananchi laki moja na Elfu ishirini na tatu watanufaika.

Itakumbukwa kuwa Eneo la Nzuguni mpaka sasa lina Visima Tisa vilivyokamilika ambavyo vina uwezo wa kuzalisha maji wastani wa lita milioni Ishirini kwa siku ambapo hadi kukamilika kwa awamu ya pili ya mradi huu itasaidia kuongeza hali ya uzalishaji maji kutoka lita milioni 81 hadi 90 kwa siku sawa na ongezeko la asiliami 30 kutoka kwenye chanzo hicho.

Mawakili ishaurini Serikali kwa weledi - Dkt. Biteko
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 16, 2025